Habari mpendwa mteja, Leo napenda tugusie kidogo kuzitambua mbao zenye dawa (treated). Wateja wengi hudhani mbao yenye dawa ni ile iliyo ya kijani kwa mwonekano lakini si sawa kwamba lazima iwe ya kijani Sana JE? TUNATAMBUAJE MBAO YENYE DAWA (TREATED) MWONEKANO (UWIANO WA RANGI) -Mbao yenye dawa rangi yake inawiana, inakua na rangi moja na si lazima iwe ya kijani sana. RANGI WAKATI WA KUICHANA- Unapoichana mbao japo itakua nyeupe kutakua na dalili inayoonyesha dawa kuingia ndani yaani haitakua nyeupe kabisa bali itawiana na rangi ya nje kuonyesha kuingia kwa dawa wakati wa kuichemsha. MAKOSA YANAYOFANYWA NA WAUZAJI WA MBAO UDANGANYIFU- Baadhi ya wauzaji wa mbao wamekua wakifanya udangayifu kwa kuweka rangi za ukili (mkeka) kwenye mbao na mbao kua na mwonekano wa kijani Sana na mteja huamini ndiyo mbao yanye dawa. WIZI- Baadhi ya wauzaji wasio waaminifu wamekua wakifanya wizi kwa namna tofauti tofauti na hili wateja wengi hulalamika. KUKOSA UAMINIFU- wauza